JE, NINAWEZA KUWA MWANACHAMA WA TUICO?

Tumekuwa tukipokea maswali mengi katika mitandao yetu ya kijamii hasa juu ya vigezo vya kuwa mwanachama wa TUICO. Sasa kupitia makala hii utapata majibu ya maswali yako yote tafadhali twende pamoja.

Wafanyakazi wa CocaCola ambao ni wanachama wa TUICO katika maadhimisho ya siku ya Mei Mosi mwaka 2019 yaliyofanyika kitaifa Jijini Mbeya.

Mfanyakazi ni nani?

Kulingana na Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za kazi Namba 7 ya mwaka 2007, Mfanyakazi ni mtu yeyote aliyeingia katika mkataba wa ajira wa aina yoyote kumfanyia kazi mtu mwingine kwa ujira.

TUICO ni nini?

TUICO ni Chama cha Wafanyakazi kinachodai, kulinda na kutetea haki, heshima na maslahi ya wafanyakazi wa Viwanda,  Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri.

TUICO wanapatikana wapi?

Makao yake makuu yapo Ilala, Dar es Salaam. Lakini TUICO ina ofisi karibu kila mkoa ndani ya Tanzania.

Ni kwa namna gani naweza kujiunga na TUICO?

Wala usihangaike ni kazi rahisi sana. Kama wewe ni mfanyakazi katika Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri tafadhali fanya yafuatayo:-

·Tembela Ofisi ya TUICO iliyoko Mkoani kwako uonane na ofisa wa TUICO ambaye atakuandikisha kuwa mwanachama kwa kujaza Fomu namba 6 kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004.

 

·Ofisa wa TUICO atakupatia kadi ya TUICO pamoja na maelezo ya ujumla kuhusu uanachama sambamba na faida za kuwa mwanachama na ushiriki wako katika Chama ili uwe mwanachama hai daima.

Bado una maswali mengine?

Na kama  bado unahitaji kujifunza zaidi kuhusu shughuli na matukio mbalimbali ya TUICO au pengine upembuzi yakinifu kuhusu chama. Mathalani, kazi zinazofanywa na chama kila siku, tafadhali tembelea tovuti yetu ya www.tuico.or.tz na katika mitandao ya kijamii tupo  (Facebook, Instagram na Twitter. Huko utapata mawasiliano mengi ya Ofisi mbalimbali za TUICO lakini pia utajisomea Katiba ya Chama, Miongozi na mambo lukuki kuhusu TUICO.

 

Karibu sana. TUICO Tunasema MSHIKAMANO DAIMA.

 


Related

Recent News 8989338124943212651

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress