TUICO Yamshukuru Rais Magufuli

Mkutano wa Baraza Kuu la TUICO-Taifa Mwaka 2020 ulifanyika katika ukumbi wa Edema Hotel mjini Morogoro siku ya Mei 31 mwaka huu. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndugu Paul Sangeze ambapo wajumbe wa mkutano huo walipendekeza maazimio mbalimbali.

Mwenyekiti wa TUICO-Taifa Ndg. Paul Sangeze akizungumza na Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la TUICO-Taifa Mwaka 2020 uliofanyika katika ukumbi wa Edema Hotel mjini Morogoro Mei 31, 2020

Wajumbe wa Baraza Kuu walimshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyoongoza katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa COVID-19. Baraza linaunga mkono kwa dhati miongozo yote anayoitoa na kuahidi kuendelea kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya ili kujikinga na janga hili.

Katika upande mwingine Wajumbe wa Baraza Kuu waliipongeza Serikali, TUICO, Waajiri kutoka Taasisi mbalimbali na Mashirikisho ya Wafanyakazi ya Kimataifa kwa hatua zote zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ikiwa ni pamoja na kuchangia kwenye Mfuko wa Maafa wa Taifa. 

Hata hivyo Chama kiliombwa kiandae mikakati ya kudumu ya kukabiliana na majanga kama ugonjwa COVID-19 yanapotokea.  Aidha Chama kihakikishe kuwa Waajiri hawatumii mazingira ya kuwepo kwa ugonjwa wa COVID-19 kukandamiza haki za wafanyakazi.

Wajumbe wa Baraza Kuu waliazimia Chama kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kiendelee kuishawishi Serikali kuridhia mapendekezo na Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambayo ina tija kwa Wafanyakazi. Mikataba hii iwe ni ile ambayo haikiuki mila na Utamaduni wa Tanzania.

Aidha, Wajumbe waliazimia Chama kiendelee kushirikiana na TUCTA na Wadau mbalimbali kuishawishi Serikali kupunguza mzigo wa Kodi kwa Wafanyakazi katika ngazi zote ili kupunguza ugumu wa maisha walionao Wafanyakazi. Aidha Wajumbe walipendekeza Serikali iendelee kuangalia uwezekano wa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi kwani kwa kipindi kirefu sasa mishahara haijaongezwa.

Hata hivyo, Baraza Kuu liliipongeza Ofisi ya Katibu Mkuu TUICO-Taifa Ndugu Boniface Nkakatisi kwa namna ilivyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa. Sambamba na hilo Baraza lilihimiza kuendelezwa kwa Umoja, Mshikano na Ushirikiano ndani ya Chama ili kuinua na kuimarisha nguvu za Chama katika kutoa huduma Bora kwa wanachama wake.

 


Related

Recent News 84378856893235987

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress