TUICO KUTETEA HAKI ZA WAFANYAKAZI KIWANDA CHA NGUO MAZAVA.
Zaidi ya wafanyakazi 2,000 walizuiliwa kujihusisha na shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha kutengeneza nguo cha Mazava mkoani Morogoro ikiwa ni kinyume na makubaliano ya kimkataba.
Licha ya menejimenti ya kiwanda kutotambua ushiriki wa TUICO kwenye mgogoro huu; Chama kinachotetea Wafanyakazi katika sekta za Viwanda, Biashara, Fedha, Huduma na Ushauri; TUICO imesalia mstari wa mbele katika kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa na wanapata wanachostahili.

Tayari mgogoro huo umeshapelekwa Tume ya Utatuzi wa Usuluhishi Mkoa wa Morogoro na usuluhishi umeendelea leo Mai 19, 2020 ingawa haukufikia maamuzi kutokana na Mwanasheria wa upande wa mwajiri kushindwa kuhudhuria.

Hatahivyo, TUICO inawawakilisha wafanyakazi wote katika mgogoro huu bila kujali kuwa baadhi yao hawajajiunga. Aidha, hili limepelekea wafanyakazi ambao sio wanachama kuomba kujiunga na Chama kutokana na kile wanachodai kupotoshwa na mwajiri wao kuwa TUICO haiwezi kuwatetea.
Mgogoro huu unakuja mara baada ya mmiliki wa kiwanda hicho kuwapa Wafanyakazi likizo ya miezi mitatu kwa madai ya kwamba kiwanda kimepoteza oda za uzalishaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi madai ambayo wafanyakazi waliyapinga.Endelea kutufuatilia kwa habari zaidi juu ya mapambano haya

Related

Regional 9111328918713986275

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress