Kwanini ni Lazima Kuimarisha Afya na Usalama Mahala pa Kazi?

Sheria ya Afya na Usalama Kazini Namba. 5 ya mwaka 2003, inatoa muongozo kuhusu mahitaji muhimu katika sehemu za kazi. Sheria hii inalenga kuzuia ajali na magonjwa sehemu za kazi ikiwa ni pamoja na kuwakinga Wafanyakazi na madhara ya kiumbo, kibaiolojia, Kemikali, Kisaikolojia, madhara ya mpangilio mpya wa kazi, madhara ya mazingira au hata VVU/UKIMWI

Wafanyakazi wakiwa katika maandamano ya Mei Mosi mwaka 2019 jijini Mbeya


Aidha, dhana ya Usalama na Afya Kazini inalenga  kulinda Usalama, Afya na Ustawi wa watu wote walio katika ajira iliyo rasmi. Suala la Usalama na Afya Kazini linajumuisha pia kuwakinga na kuwalinda wafanyakazi wengine, wanafamilia, waajiri, wateja, watoa huduma pamoja na jamii iliyozunguka, ambao kwa njia moja au nyingine wanaweza kudhurika na mazingira ya sehemu ya kazi.

Pia dhana hii inalenga kuhakikisha kuna mazingira huru yasiyo na ajali, mikwaruzo ya mwili na kudondokewa na vitu. Pia maumivu yatokanayo na michubuko au mikwaruzo ni matokeo ya mara mtu anapoumia au madhara yanayotarajiwa baada ya mfanyakazi kuumia.

Wafanyakazi wengi pia hupata madhara makubwa na hata kufa endapo vitu vyenye ncha kali au vitu vinavyofanana na hivyo vinapowaangukia kichwani ikiwa mfanyakazi hakuvaa vifaa vya kinga (Protective gears). Ndio maana TUICO tunapigania sana kuhakikisha waajiri wanawapatia wafanyakazi wao kinga ili kulinda maisha yao.

Kwa upande mwingine, dhana ya afya na Usalama hulenga mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja:

  • Kuweka na kuboresha mazingira mazuri yatakayopelekea ustawi wa wafanyakazi wote kimwili na kiakili. 
  • Kuwakinga wafanyakazi na madhara yatokanayo na Afya na Usalama yanayoweza kuwasababishia kuacha kazi.
  •  Kuwakinga wafanyakazi katika ajira zao kutokana na madhara ya kiafya yanayoweza kuwakabili
  •  Kuweka na kuhakikisha mfanyakazi anayaelewa na kuyakabili maeneo yake ya kazi kimazingira na kisaikilojia.

Kwanini TUICO tumeanzisha mpango wa kuimarisha Afya na Usalama Mahala pa Kazini?

Kuna mambo mengi yanayosababisha kuwepo kwa mpango huu, lakini yafuatayo ni baadhi tu:-

·Kimaadili, mfanyakazi hapaswi kuwa katika mazingira yatakayohatarisha maisha yake binafsi awapo kazini na hata wengine wanaomzunguka.

·Kiuchumi, Serikali nyingi zinatambua kwamba Usalama na Afya duni kazini unapelekea hasara kwa Taifa. (mfano, Serikali huingia gharama kuwatibu, kuwahudumia majeruhi, kuwalipa fidia na mfanyakazi kushindwa kufanya kazi tena).

·Kisheria, Mahitaji ya Afya na Usalama Kazini yameainishwa na Sheria ya Madai na Sheria ya Jinai.

Bila shaka pasipokuwa na msisitizo wa kisheria sehemu nyingi za kazi hazitaweza kutekeleza majukumu yake ya kuimarisha suala la Usalama na Afya kwa Wafanyakazi ipasavyo. Moja ya madhumuni ya Shirika la Kazi Duniani ILO ni kusimamia Viwango vya Kimataifa vya Kazi na Ustawi wa Wafanyakazi ambapo pia sisi TUICO tunahakikisha kunakuwa na viwango vyema mahala pa kazi.

 


Related

Recent News 8194942929894522618

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress