TUICO: Changamoto za Wafanyakazi Bado Kizungumkuti

Hali ya sasa ya wafanyakazi nchini Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla, inatokana na mapambano yaliyoendeshwa na wafanyakazi na vyama vyao enzi za zamani ya kudai haki na masilahi yao. Mapambano haya hayawezi kusahaulika na tunayaendeleza kwa wakati wote. Ndio maana bado tuna maadhimisho kama vile ya Mei Mosi sambamba na vyama mbalimbali vya wafanyakazi ambavyo vimeendelea kudai, kutetea na kulinda haki, heshima na masilahi ya wafanyakazi.

Wafanyakazi wa kiwanda cha Mazava mkoani Morogoro. Walikumbwa na janga la kutaka kupewa
likizo ya miezi mitatu pasipo malipo hali ambayo ni kinyume na kanuni na miongozo ya kazi.

Hatahivyo, licha ya mafanikio kadhaa katika  sekta ya kazi, bado tabaka la wafanyakazi duniani linakabiliwa na changamoto mbalimbali huku ukosefu wa ajira ukiwa ni miongoni mwa changamoto hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinazowakabili vijana. Bapo kuna vijana wanaohitimu mafunzo kila mwaka, lakini hawapati ajira. Wengi wapo mitaani na wengine wameingia kwenye sekta ya uchumi isiyo rasmi.

Kwa upande mwingine, wafanyakazi bado wanakabiliwa na tatizo la vipato duni. Bado kipato ni kidogo ambacho hakikidhi mahitaji yao ya kila siku. Sambamba  na hilo bado waajiri wana mazingira ambayo ni hatarishi kwa wafanyakazi kwani waajiri kadhaa bado hawawapi waajiriwa wao vifaa sahihi vya kinga na vya kufanyia kazi hali ambayo ni kinyume na kanuni na sheria zinazoongoza mawanda ya kazi hasa kwenye afya na usalama mahali pa kazi.

Hatahivyo, kuna waajiri wakorofi wasiopenda wafanyakazi wao wajiunge na vyama vya wafanyakazi. Baadhi yao wanawazuia wafanyakazi kujiunga kwenye vyama vya wafanyakazi kwa kutishiwa kufukuzwa kazi. Kulingana na Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazini ya mwaka 2004  Kifungu cha 9, kinatoa haki kwa mwajiriwa kuwa na haki ya kuunda na kujiunga na vyama vya wafanyakazi sambamba na kushiriki katika kazi halali za chama cha wafanyakazi.

Katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Covid-19, kuna waajiri ambao wamelitumia kama kigezo cha kukiuka haki za wafanyakazi kwa kutaka kuwapa likizo zisizo na malipo au kuwapunguza pasipo kuzingatia kanuni na miongozo mbalimbali ya ajira. Hatahivyo, TUICO imeendelea kuhakikisha haki, heshima na masilahi yao yanabaki salama. 

TUICO tunaendelea na juhudi zetu za kudai, kutete na kulinda haki, heshima na masilahi ya wafanyakazi wa sekta ambazo kwazo tunasajili wanachama huku tukizingatia sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza mawanda ya ajira na mahusiano kazini hapa Tanzania.


Related

Recent News 6947309900439891129

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress