TUICO Kuna Uhakika wa Utetezi wa Changamoto za Mahala pa Kazi

TUICO ni chama cha wafanyakazi cha kipekee sana hapa chini Tanzania. TUICO imeanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa madhumuni mbalimbali ambayo yamefafanuliwa kikamilifu katika Katiba ya yake, sura ya pili (2:1) ambayo ni pamoja na:-
Kuboresha na kuendeleza hali nzuri ya
wanachama katika maisha yao wakiwa kazini.
Kushirikiana na kujadiliana na waajiri
katika kuunda kamati za majadiliano na kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi
ili kudumisha amani mahali pa kazi.
Kujadiliana na kuondoa tofauti
zinazojiotokeza baina ya mwajiri na mwanachama au Mwanachama mmoja na mwingine
kwa njia ya makubaliano ya amani kila itakapowezekana
![]() |
Kujadili, kufunga na kusimamia
utekelezaji wa mikataba ya Hali Bora za kazi. Aidha kushirikiana na wahusika
wengine katika kusimamia utekelezaji wa TUZO, Kanuni za Utumishi na Sheria
nyingine za kazi zitumikazo nchini.
Kushirikiana na kubadilishana ujuzi na vyama
vingine vya wafanyakazi nchini pamoja na vile vya kimataifa.
Kuwasiliana na Serikali kuhusu haja ya
kutunga Sheria sahihi za Kazi na kuandaa Sera za kuendeleza uchumi na maisha ya
jamii.
Kulinda maslahi ya Wanachama kwa kusaidia Serikali kuepukana na Uandaaji wa Sera ambazo hazina manufaa kwa Wafanyakazi.
TUICO imeendelea kusimamia msingi wa
Haki, Heshima na Masilahi ya wafanyakazi kwa kuhakikisha tuyanadai, tunayalinda
na kuyatetea ili kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa katika mazingira ambayo ni
rafiki na yasiyo ya hatari kwao.
Aidha, kama chama TUICO tumeendelea
kuhakikisha tunafanya mazungumzo ya pamoja kati ya mwajiri na mfanyakazi, ikiwa
ni katika kuhakikisha kunakuwa na mahusiano mema kati ya pande zote mbili.
Tumeshirikiana na serikali katika
kutatua migogoro katika maeneo mbalimbali, huku mingine ikisababishwa na
changamoto za majanga kama ugonjwa wa Covid-19 ambalo kwa kiasi kikubwa
limeathiri mifumo ya maisha hasa katika sekta ya viwanda, Biashara na
kadhalika.
Huu ni wito kwa wafanyakazi kutoka sekta
ya viwanda, biashara, taasisi za fedha, huduma na ushauri wajiunge na TUICO ili
waendelee kufurahia uanachama wenye uhakika wa utetezi pale changamoto za
ajira zinapojitokeza. TUICO tunaishi
kwenye sheria na miongozo mbalimbali inayoongoza kada ya ajira hapa nchini na
mikataba mingine ambayo tumeridhia kama
taifa.
MSHIKAMANO
DAIMA.