Ukatili wa Kijinsia Uliongezeka kwa Asilimia 39

Ukatili na udhalilishaji kwenye maeneo ya kazi huathiri saikolojia, afya ya kimwili, kijinsia na hata katika mazingira ya familia na jamii. Udhalilishaji pia huathiri ubora wa huduma za umma na binafsi, na zinaweza kuzuia watu, hasa wanawake, kupata haki zao katika ulimwengu mzima wa ajira.


Ukatili hauendani kabisa na shughuli za biashara. Ni kikwazo kikubwa katika uchumi endelevu na huathiri vibaya mazingira ya kazi, mahusiano, ushiriki na maslahi ya wafanyakazi mahala pa kazi. Ndio maana ni wajibu wa kila mmoja kupaza sauti yake dhidi ya ukatili wa kijinsia katika jamii na maeneo ya kazi.

Nchini Tanzania, kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba mwaka 2016, zaidi ya matukio milioni 2 na laki 8 ya uhalifu ukiwemo ukatili yaliripotiwa katika vituo vyote vya Polisi nchini ukilinganisha na kesi milioni 1 na zaidi ya laki 9 zilizoripotiwa katika kipindi cha mwaka 2015. Hilo ni ongezeko la kesi zaidi ya kesi laki 9 ambazo ni sawa na asilimia 49. 

Kwa kipindi hicho, jamii imeendelea kushuhudia vitendo vya ukatili wa kijinsia. Mwezi Januari hadi Disemba mwaka huohuo, jumla ya kesi elfu 31 za unyanyasaji wa kijinsia ziliripotiwa ikilinganishwa na kesi elfu 23 zilizoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka uliopita. Hili ni ongezeko la kesi zaidi ya 8,000, sawa na asilimia 39 ya kesi za mwaka 2015.

Mathalani,  mikoa ya polisi hapa nchini yenye idadi kubwa ya waathirika wa ukatili wa kijinsia kwa kipindi cha mwaka 2016 ilikuwa Temeke (4,101), Morogoro (3,073), Singida (2,567), Arusha (2,190) na Tanga (1,904) huku kesi za lugha ya matusi zikiwa ni zaidi ya 3000.

Takwimu hizi zinaonesha hali halisi ya ukatili wa kijinsia katika jamii na maeneo ya kazi. Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), kinaungana na jamii na wadau mbalimbali katika kampeni za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye jamii yetu na hasa katika maeneo ya kazi.

Wafanyakazi wapewe likizo za uzazi pasipo kukalipiwa kwa lugha za ukatili. Wafanyakazi wasibaguliwe kwa sababu ya jinsi zao. Tunahitaji mazingira rafiki kwa wafanyakazi wote.


Related

Women 7163948185370528187

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress