Wafanyakazi 29 Wajiunga na TUICO

Mapema leo Julai 23, 2020 wafanyakazi 29 wa Big Bon Petroleum Limited Dar es Salaam vituo vya Temeke na Mbagala wamejiunga na Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO).

Viongozi wa TUICO na wanachama wapya kutoka Big Bon Petroleum Limited kituo cha Mbagala

Hatua hii inakuja ikiwa ni takribani mwezi mmoja umepita baada ya TUICO ikishirikiana na vyama kadhaa vya wafanyakazi kufikia makubaliano yenye tija kwa wafanyakazi. Waajiri wa makampuni matatu likiwemo Big Bon Petroleum Limited walitangaza likizo kwa wafanyakazi wao 39 pasipo malipo hali iliyosababisha taharuki kwa wafanyakazi hao.

Kufuatia makubaliano hayo, wafanyakazi 39 walipewa likizo (garden leave) ya miezi mitatu yenye malipo, iliyoanza Juni Mosi hadi Septemba Mosi, 2020 kwa sababu za kupungua kwa kazi kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19 ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa na kusababisha kazi nyingi kusimama.

TUICO kimeendelea kuwa chama cha wafanyakazi ambacho kinasimamia msingi wa haki, heshima na maslahi ya wafanyakazi. Kimeendelea kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu haki zao za msingi. Aidha, kimefanya utetezi kwa maelfu ya wafanyakazi nchini na kusimamia ustawi wa mazingira yao ya kazi.


Related

Recent News 3385331472068522498

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress