Wafanyakazi Kuweni Wazi Kuripoti Changamoto Kwenye Maeneo ya Kazi

Lengo nambari 8 la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ni kuchagiza ukuaji endelevu, jumuishi wa uchumi na ajira zenye hadhi kwa wote. Na moja ya mambo ya msingi kwenye lengo hili ni kulinda haki za nguvukazi na kuhakikisha mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote, pamoja na wale walio kwenye ajira ambazo zina hatari nyingi.

Viashiria vya ufikiwaji wa lengo hili ni pamoja na kuongezeka kwa ufwatwaji wa haki za kazi sambamba na uhuru kwa wafanyakazi kujumuika ikiwa ni pamoja na kuunda na kujiunga na vyama vya wafanyakazi na kupata mikataba ya hali bora.

Umoja wa Mataifa unasema wafanyakazi wengi ulimwenguni kote wanakabiliwa na hatari nyingi kwenye maeneo yao ya kazi. Kulingana na takwimu za hivi karibuni kutoka kwa nchi 55, (median) vifo 3 vilitokea kwa wafanyakazi 100,000 na majeruhi (non-fatal injuries) 889 waliripotiwa kwa wafanyakazi 100,000. Hii sio taarifa njema mahala pa kazi.

Wafanyakazi wa kawaida katika eneo la ujenzi. Uvaaji wa  gia za kinga ni muhimu, kwani  huepusha madhara mbalimbali maeneo ya kazi. 

Nchini Tanzania, lengo la maendeleo mtambuka ni kuboresha hali ya kazi kwenye vituo vyote, kupitia utoaji wa huduma bora za Afya na Usalama Kazini (OHS) ili kuondoa hatari kazini sambamba na uimarishaji wa sekta zote za uzalishaji na za huduma kama iliyokusudiwa katika Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025.

Sera ya Kitaifa ya Afya na Usalama ya Kazini inaweka wazi kwamba waajiri watahakikisha afya na usalama kazini, uundaji wa kamati za afya na usalama mahali pa kazi, watafanya mafunzo sambamba na kuripoti ajali zinazotokea kazini, magonjwa na matukio mengine hatarishi kwa mamlaka husika wakati wafanyakazi wataunda na kushiriki kwenye kamati za afya na usalama mahali pa kazi, wataripoti hali yoyote ambayo ni hatarishi kwa mamlaka husika na kuzingatia mahitaji ya afya na usalama kazini.

Kama chama cha wafanyakazi kinachoongoza hapa nchini, TUICO kimekuwa kikipaza sauti ya haki kwa wafanyakazi. TUICO imefunga mikataba ya Hali Bora na kujadiliana na waajiri juu ya hatima za wafanyakazi. Aidha, kimefanya utoaji wa elimu kwa wafanyakazi wa sekta za viwanda, biashara, fedha na huduma na ushauri kuhusu umuhimu wa vyama vya wafanyakazi na afya na usalama kazini.

TUICO inatoa rai kwa wafanyakazi wote kuwa wawazi na kuripoti changamoto kwenye maeneo yote ya kazi. Usalama wa wafanyakazi ni muhimu kuliko kazi wanazofanya. Tunatoa wito kwa waajiri kuhakikisha wafanyakazi katika huduma za ujenzi wanakuwa na kinga kwa ajili ya usalama wao. Walakini, waajiri lazima wafuate sheria na kanuni mbalimbali ambazo zimeanzishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia Miongozo na Chama cha Waajiri Tanzania.


Related

Recent News 7920877273866457230

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress