Wanawake Wajengewa Uwezo Kukabiliana na Changamoto Mahala pa Kazi.

Wafanyakazi wanawake wanakumbana na changamoto nyingi ukiwemo ukatili na udhalilishaji wa kijinsia. Wapo wanawake ambao wamenyimwa likizo za uzazi kutokana na uwepo wa waajiri ‘wakorofi’ lakini pia malipo duni. Hali hii inaisukuma Idara ya Wanawake TUICO Makao Makuu kufanya vikao vya mara kwa mara na kamati za wanawake kwenye matawi.

Wajumbe wa Kamati ya Wanawake TUICO-TANESCO Makao Makuu wakishiriki kikao kilichoratibiwa na Idara ya Wanawake TUICO Makao Makuu kujadili masuala yanayohusu wanawake na ustawi wao  maeneo ya kazi.

Ikumbukwe kuwa TUICO inafanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali kwenye matawi yake nchi nzima. Hivyo, Idara ya Wanawake, Afya na Usalama na Mazingira makao makuu, inatekeleza vikao hivi na kamati za wanawake ili kuwajengea wanawake uwezo wa kukabiliana na changamoto mahali pa kazi na hatimaye ustawi.

“Tunafanya vikao na wajumbe wa kamati za wanawake ili kuwajengea uwezo viongozi wapya waliochaguliwa kujua majukumu yao na namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba wanawake mahala za kazi.” Maria Bange Mkuu wa Idara ya Wanawake, Afya na Usalama na Mazingira, TUICO Makao Makuu.

Kamati za wanawake kwenye matawi ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) zipo chini ya Idara ya Wanawake, Afya na Usalama na Mazingira ambayo  inahusika na kuratibu na kusimamia wafanyakazi wanawake, wanachama na watu wenye ulemavu. Idara imekuwa ikihamasisha waajiri na wafanyakazi kuzingatia na kudumisha afya na usalama maeneo ya kazi.


Kupitia idara hii, TUICO imeunda kamati za wanawake takribani 400 na zaidi ya kamati 570 za afya na usalama katika matawi yake ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa chachu ya maendeleo na ustawi wa wanawake mahala pa kazi.


Related

Women 6551148858735836186

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress