TUICO YATAFAKARI CHANGAMOTO KWA VIJANA ULIMWENGU WA KAZI

Katika kuadhimisha Siku ya
Kimataifa ya Vijana jana Agosti 12, 2020, TUICO iliungana na Jumuiya ya
Kimataifa kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kufanya shangwe katika ofisi za
Makao yake Makuu zilizopo Ilala, Dar es Salaam ambapo vijana walikuja pamoja kwa
kuimba nyimbo za mshikamano na vionjo vingine ikiwa ni katika kutambua mchango
wao mkubwa katika ulimwengu wa kazi duniani.
![]() |
Maafisa wa TUICO wakiwa katika picha na wafanyakazi wa kiwanda cha Afri Tea and Coffee Blenders Ltd. cha Dar es Salaam. Agosti 12, 2020 |
TUICO, haikuishia hapo,
ilipata wasaa wa kutembelea kiwanda cha Afri Tea and Coffee Blenders Ltd.
kilichopo Jijini Dar es Salaam ambapo pia ilikutana na vijana ambao ni
waajiriwa katika kiwanda hicho. TUICO iliwaeleza maana na umuhimu wa siku ya
kimataifa ya vijana lakini pia iliwahakikishia vijana hao kuwa inatambua
mchango wao katika kuleta mabadiliko ya kiulimwengu.
Maria Bange, ambaye ni
Mkuu wa Idara ya Wanawake, Walemavu, Afya na Usalama TUICO Makao Makuu
aliyeongoza msafara wa jana, aliwaeleza vijana kuwa katika kusherehekea siku
hii kwa mwaka 2020, “TUICO Tukiungana na vyama vingine vya wafanyakazi duniani,
tunahamasisha kazi zenye staha, salama na za kudumu kwa watu wote”.
Changamoto za afya na
usalama mahala pa kazi na mikataba mibovu zimekuwa zikijitokeza katika maeneo
mbalimbali Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla. “Hivyo, siku ya vijana
inatupa wakati wa kufatakari nafasi ya vijana wakiungana na
vyama vya wafanyakazi katika kupambania kazi zenye staha, salama na
za kudumu kwa watu wote na haki zingine za wafanyakazi.” alisema Bi. Maria.
MSHIKAMANOOOOOOOOO
ReplyDelete