Zaidi ya Wafanyakazi 10 wa Yaohui Furniture Wajiunga na TUICO

Jana tulikuwa na wakati mzuri na wafanyakazi wa YAOHUI FURNITURE huko Mbezi- Tangi Bovu, Dar es Salaam. Tulizungumza nao juu ya umuhimu wa vyama vya wafanyakazi.
![]() |
Tulisisitiza faida ya Mkataba wa Hali Bora. Kwa kuwa sheria
haisemi kila kitu ambacho wafanyakazi wanapaswa kufaidika mahali pao pa kazi,
Mkataba wa Hali Bora unafafanua zaidi ya sheria. Tunafurahi kwamba wafanyakazi
walikuwa tayari kabisa kujiunga na vyama vya wafanyakazi. Zaidi ya wafanyikazi
10 walionyesha nia ya dhati kabisa kujiunga na TUICO.
Mkataba wa Hali Bora huleta uhusiano mzuri kwenye maeneo ya kazi. Ni mkataba muhimu hasa kwenye usimamizi wa kazi na unawarahisishia waajiri, vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wenyewe juu ya namna wanavyoshirikiana mahali pa kazi na matokeo ya baadaye na kwahiyo mkataba wa Hali bora unabaki kuwa kiungo muhimu katika mafanikio mahala pa kazi.
Aidha, mkataba wa hali bora, unatafsiri utendaji thabiti wa
kampuni au taasisi, unapunguza utoro, kuongezeka kwa ufanisi, tija kubwa na
hutengeneza mazingira ya ubunifu kuwahamasisha wafanyakazi kwa kuongeza uaminifu
wa mfanyakazi. Hapo jana tuliwaambia wafanyakazi wa YAOHUI FURNITURE wajiunge
nasi ili wafaidike na mikataba hii na wasaidiwe wakati changamoto zingine zinapotokea
mahali pao pa kazi.
Kwa mifano dhahiri, tulihubiri jinsi TUICO ilivyojitahidi
hadi kusainiwa kwa mkataba wa hali bora na Lake Cement Ltd, TANESCO na vile
vile jinsi tulivyotatua migogoro kama ile ya Mazava Fabrics and Production East
Africa kule Morogoro.