Siku ya Walemavu Duniani: 15% ya Watu Duniani ni Walemavu

Desemba tatu kila mwaka, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu. Takwimu za Benki ya Dunia (WB), zinaonesha kuwa asilimia 15 ya idadi ya watu wote duniani wana aina fulani ya ulemavu na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea.
Moja ya tano ya idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa na aina fulani ya ulemavu ambao ni karibu watu milioni 200, wana ulemavu mkubwa. Yaani, kati ya watu watano wenye aina fulani ya ulemavu duniani, mmoja ana ulemavu mkubwa. Kote duniani, walemavu wanakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo za elimu duni, kukosa huduma za afya, ujira mdogo sambamba na kiwango kikubwa cha umasikini.
![]() |
Modibo Sall (10) akimfundisha baba yake Amadou (52) lugha ya ishara. Modibo alizaliwa kiziwi. Anaishi kijiji cha Bouake’, nchini Ivory Coast. Picha na UNICEF|Frank Dej |
Siku hii inatukumbusha umuhimu wa kuwajumuisha watu wenye ulamavu katika
mambo mbalimbali yakiwemo ajira zenye utu,
michezo, maamuzi, afya na elimu.