TUICO Yafanya Uchaguzi wa Kamati ya Vijana na Wanawake

Desemba 17 na 18, 2020 TUICO imefanya uchaguzi wa Kamati zake mbili, Kamati ya Vijana na Kamati ya Wanawake TUICO Taifa. Katika uchaguzi wa Kamati ya Vijana TUICO Taifa, Ndg. Allen Lyimo alishinda kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hadi 2025. Allen ni mfanyakazi wa kiwanda cha Sunflag Limited, mkoani Arusha.
Akiwashukuru wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Vijana, Allen alisema atajikita zaidi katika kufanya mambo yanayoonekana huku akisema atatumia uzoefu alionao kuwainua vijana ndani ya chama sambamba kuwahamasisha wengine ambao ni wafanyakazi kujiunga na TUICO.
Walakini, Desemba 18, 2020 Bi. Zeralucy Masanja, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUICO Taifa. Bi. Zeralucy ambaye ni mfanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alifanikiwa kutetea nafasi yake kwa miaka mitano mingine. Zeralucy aliahidi kupigania masilahi ya wanawake ndani ya TUICO.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Bi. Zeralucy Masanja akipongezwa na Katibu Mkuu Msaidizi wa TUICO Taifa Ndg. Tamim Salehe baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo Desemba 18, 2020 | Morogoro |
Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndg. Paul Sangeze aliwaasa viongozi watakaochaguliwa kujenga umoja na mshikamano ndani ya TUICO ili chama kiendelee kudumu. Aliongeza kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kubadilisha mtazamo wa wanawake wengine nchini kuhusu vyama vya wafanyakazi.
![]() |
Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndg. Paul Sangeze akizungumza wakati wa Mkutano wa Uchaguzi wa Kamati ya Wanawake TUICO Taifa uliofanyika Desemba 18, 2020 - Morogoro |
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TUICO Taifa, Ndg. Boniface Nkakatisi alisema
uongozi ni utumishi hivyo ni lazima viongozi wanaochaguliwa ndani ya chama wawe
watumishi wa wengine ili chama kiendelee kudumu. Aidha, Nkakatisi aliongeza
kuwa sasa zama zimebadiliaka, ni lazima vijana wafanye mambo yao kwa hoja
katika suala zima la kupigania, kutetea na kulinda haki, heshima na masilahi ya
wafanyakazi.
![]() |
Katibu Mkuu wa TUICO Taifa Ndg. Boniface Nkakatisi akizungumza wakati wa Mkutano wa Uchaguzi wa Kamati ya Vijana TUICO Taifa uliofanyika Desemba 17, 2020 - Morogoro |