KUT Yajadili Bajeti ya TUICO 2021

 

Kamati ya Utendaji TUICO Taifa (KUT) leo Jumanne, Januari 26, 2021 imepitia na kujadili bajeti a Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kwa mwaka 2021 ambayo inatarajiwa kupitishwa na Baraza Kuu.

Wajumbe wa KUT wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa kufunga kikao cha Kamati hiyo Januari 26, 2021, Morogoro | Venance Majula/TUICO

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Morogoro, Naibu Katibu Mkuu wa TUICO Taifa Ndg. Tamim Salehe ambaye pia ni Mjumbe wa KUT ameeleza baadhi ya changamoto zilizojitokeza mwaka 2020.

 “Mnafahamu kwamba kumekuwa na changamoto ya Covid-19. Kuna makampuni mengi yalifunga, wafanyakazi walifanya kazi wakiwa nyumbani na wengine walipunguzwa kabisa,” alisema Ndg. Tamim

Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndg. Paul Sangeze amewashukuru Wajumbe wa KUT na kuwatakia safari njema wakati wakirejea kwenye maeneo yao ya kazi,”

“Kwanza nimshukuru Mungu. Ninawashukuru wajumbe wote kwa michango yenu. Nimshukuru Katibu Mkuu na Wajumbe wake kwa semina ya jana. Naamini ile semina imetupeleka mahala,” alisema Ndg. Sangeze.

Aidha, Sangeze amesisitiza umoja na mshikamano ndani ya TUICO huku akikipongeza chama na Mkutano Mkuu kwani idadi kubwa ya wajumbe wa KUT ni wanawake. Amesema uwepo wa vijana na wanawake kwenye KUT ni miongoni mwa mageuzi makubwa katika historia ya vyama vya wafanyakazi hususani TUICO.

“Tuishi kama ndugu wanaonia mamoja. Miaka mitano ni mingi mno na ni michache mno. Naamini tukianza vizuri, tutamaliza vizuri. KUT ina akina mama saba na akina baba watano. Hii ni ishara fulani. Haijawahi kutokea katika historia ya TUICO. Ni hatua kubwa sana,” aliongeza Ndg. Sangeze

Kwa mwaka 2021, TUICO imejipanga kufanya uhamasishaji, elimu, mikataba ya hali bora, utetezi zaidi, lakini pia, kuimarisha na kukuza shughuli zake pamoja na kutoa huduma bora kwa wanachama ili ifikie dhamira yake ambayo ni kuwa chama imara na cha kidemokrasia kinachotoa huduma bora kwa Wanachama wake.

 

Related

Women 2939455330731128452

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress