Serikali Yazindua Mpango Kazi Kushughulikia Migogoro ya Kazi Nchini

 

Serikali leo Ijumaa, Januari 29, 2021 imezindua Mpango Kazi wa Kusikiliza na Kushughulikia Malalamiko ya  Wadau na Kikosi Kazi cha Ukaguzi Maalumu katika sekta ya kazi na ajira. Mpango huo umezinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika hafla iliyofanyika ukumbi wa NSSF, Morogoro.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mhagama amesema lengo la mpango huo ni kuwawezesha wafanyakazi, waajiri na wananchi kwa ujumla kufahamu mamlaka sahihi zinazosimamia sheria zao na mamlaka sahihi zinazopokea malalamiko yao ni kupunguza migogoro ya wafanyakazi katika ulimwengu wa kazi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi  wa Mpango Kazi wa kushughulikia na kusikiliza malalamiko ya wadau na kikosi kazi cha cha ukaguzi maalumu katika sekta ya kazi na ajira, Jan 29, 2021, Morogoro | Venance Majula/TUICO

“Mpango kazi una lengo la kuwawezesha wafanyakazi, waajiri na wananchi kwa ujumla kufahamu mamlaka sahihi, kwanza zinazosimamia sheria zao, na mamlaka sahihi  zenye wajibu wa kupokea malalamiko yao,” alisema Waziri Mhagama.

Aidha, Mhe. Mhagama amebainisha kuwa ujio wa mpango huo ambao unakuwa kliniki ya migogoro ya kazi, unaowaleta pamoja wafanyakazi kupitia TUCTA, waajiri kupitia ATE pamoja na serikali, sio mbadala wa maamuzi za usuluhishi zilizopo nchini, bali unalenga kubaini maeneo yenye changamoto na kutoa elimu sahihi ili kupata suluhu ya kudumu.

Katika uzinduzi wa kliniki hiyo ya kazi inayotarajiwa kufanya kazi mikoa yote nchini kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi, Mhe. Mhagama amewataka wadau katika maeneo ya kazi kuaminiana na kuwa kitu kimoja ili kuhakikisha uzalishaji unakuwa wa ufanisi kwa manufaa ya pande zote zinazohusika.“Kuna haja ya kubadilisha mindset [mtazamo], waajiri wasiwaogope wafanyakazi wala vyama vya wafanyakazi. Na vyama vya wafanyakazi visiwaogope waajiri. Hapo bado kuna gap [ombwe], waajiri wanaona vyama vya wafanyakazi kama ni maadui. Lakini ni lazima tujue sababu ni nini – tupate sababu hiyo tushughulike nayo,” aliongeza Mhe. Mhagama.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare ameishukuru Wizara ya Kazi kwa kupanga semina hiyo ifanyike mkoani Morogoro. Amesema hii ni fursa ya kutatua kero na changamoto za kazi zilizopo mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare katika uzinduzi wa mpango kazi wa kusikiliza na kushughulikia malalamiko ya wadau sekta ya kazi na ajira, Jan. 29, 2021, Morogoro | Venance Majula/TUICO

“Semina hii itaweza kutusaidia kuimarisha mahusiano kati ya wadau wote. Yaani kutatua shida na changamoto zote zitakazokuwepo,” alisema Mhe. Ole Sanare

Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA) Ndg. Tumaini Nyamhokya amewataka viongozi wa vyama wa wafanyakazi nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wafanyakazi kuhusu mpango huu.

Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ndg. Tumaini Nyamhokya Jan. 29, 2021 | Venance Majula/TUICO

“Viongozi wa wafanyakazi tutoe elimu nzuri sana kwa wafanyakazi, wasije wakafiri hii kliniki ya kusikiliza na kutetea wafanyakazi, imekuja kuwa mbadala wa ule mfumo mzima wa ukataji wa rufaa za wafanyakazi. Kwa hiyo, ipo CMA, ipo Mahakama Kuu - Lakini kwenye hatua za awali kabla tatizo halijawa kubwa, basi wafike kwenye kliniki hii. Huenda tatizo likatatuliwa kabla halijafika mahakamani,” alitanabaisha Nyamhokya

Naye Dkt. Aggrey Mlimuka - Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) amesema mpango huu unafaida kwa pande zote tatu.

Dkt. Aggrey Mlimuka - Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Jan 29, 2021 | Venance Majula/TUICO

“Amani sehemu za kazi inatunufaisha wote. Wafanyakazi watapata huduma zaidi, waajiri watapata kipato zaidi, serikali nayo itapata kipato zaidi ili ifanye miradi yake zaidi,” alisema Dkt. Mlimuka.

Kwa upande wake Ndg. Maridadi Phanuel, Mratibu wa Taifa wa Sheria za Kazi - Shirika la Kazi Duniani (ILO-Tanzania), kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika hilo ukanda wa Afrika Mashariki, amesema ILO itaendelea kushirikiana na wadau wote nchini ili kuhakikisha kunakuwa na kazi zenye staha.

Ndg. Maridadi Phanuel, Mratibu wa Taifa wa Sheria za Kazi - Shirika la Kazi Duniani (ILO-Tanzania), Jan. 29, 2021 | Venance Majula/TUICO

“Utatuzi wa migogoro unatakiwa kuwa wa wakati na kwa kufuata utaratibu ili kuhakikisha pande husika wanakuwa na mahusiano mema. Kuweka namna ya kupokea malalamiko sehemu za kazi na kuhakikisha malalamiko hayo yanashugulikiwa ipasavyo na kwa utaratibu ili kuhakikisha kunakuwa na kazi za staha,” alisema Ndg. Maridadi

Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndg. Paul Sangeze (kulia), Katibu Mkuu wa TUICO (katikati) na Mwenyekiti wa Kamati (wing) ya Wanawake TUCTA na Katibu wa TUICO Mkoa wa Singida  (kushoto) wakishiriki uzinduzi wa mpango kazi wa kushughulikia malalamiko ya wadau sekta ya kazi na ajira, Jan 29, 2021, Morogoro | Venance Majula/TUICO

Miongoni mwa waliohudhuria uzinduzi wa mpango huo ni pamoja na Katibu Mkuu wa TUCTA Ndg. Said Wamba, Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa TUICO Ndg. Paul Sangeze na Ndg. Boniface Nkakatisi, mtawalia - pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake TUCTA ambaye pia ni Katibu wa TUICO Singida, Bi Rehema Ludanga.

Related

Sectoral 8503253842398602219

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress