Sangeze: Ni Wakati wa Kuwajibika Zaidi

 

Mweyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) Ndg. Paul Sangeze, leo Jumatano, Januari 27, 2021 amefungua kikao kitakachotathmini na kupanga mpango mkakati wa TUICO.

Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndg. Paul Sangeze akifungua kikao cha tathmini ya mpango mkakati wa chama 2021-2025, Januari 27, 2021, Morogoro | Venance Majula/TUICO

Akifungua kikao hicho, Sangeze amewataka watumishi wote wakiwemo makatibu wa sekta, idara na vitengo; makatibu wa kanda na mikoa; pamoja na watendaji wote kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa ufanisi katika utekelezaji wa mpango kazi wa TUICO unaopangwa. 

“Kupanga mpango ni jambo moja na utekelezaji ni suala jingine. Hatupaswi hata kidogo kufumbia macho pale inapoonekana mmoja wetu anahujumu utekelezaji wa mpango kazi utakaopangwa kwa uzembe na kwa kutotimiza wajibu,” alisema Sangeze. 

Sangeze ameongeza kuwa mahitaji ya chama kiuendeshaji ni makubwa. Wanachama na watendaji wana matarajio makubwa kimafanikio kutoka TUICO. Hivyo amesisitiza umoja, mshikamano, uwazi na uwajibikaji kwa kila mmoja ili kuakisi mwelekeo na  mahitaji ya chama. 

“Tuanze pamoja kwa malengo makubwa na tumalize pamoja kwa mafanikio makubwa,” aliongeza Sangeze. 

Kwenye kikao hicho cha siku tatu, kinachofanyika mkoani Morogoro, pamoja na mambo mengine wajumbe watafanya tathmini ya mpango mkakati wa TUICO uliomalizika Disemba 2020  na kupanga mpango kazi mwingine kwa mwaka 2021-2025. 

“Hiki ni kikao muhimu sana kwa chama chetu. Hapa tutafanya tathmini ya mpango mkakati wa Julai-Disemba, 2020 na kupanga mpango mkakati wa miaka mitano 2021-2025 na mpango mkakati wa Januari-Disemba, 2021. Kwa hiyo wajumbe tuwe wawazi na wakweli,” alisema Naibu Katibu Mkuu (TUICO), Ndg. Tamim Salehe. 

Naibu Katibu Mkuu wa TUICO Taifa Ndg. Tamim Salehe akizungumza wakati wa kikao cha tathmini ya mpango mkakati wa chama 2021-2025, Januari 27, 2021, Morogoro | Venance Majula/TUICO

Kwa niaba ya wajumbe, Katibu wa TUICO Mkoa wa Iringa na Njombe Ndg. Karim Bachalla alitoa salamu za wajumbe ambapo alisema wanakubaliana na maneno ya Mwenyekiti na wako tayari kuhakikisha chama kinanufaikia na mpango mkakati unaopangwa mwezi huu. 

“Tunakubalina na wewe kabisa, kwamba chama kutokuwa na mpango mkakati ni sawa na kuwa mfu. Kwa hiyo tutapanga mpango mkakati utakaokuwa na manufaa kwa chama. Tunaendelea kusisitiza, tutapanga mambo yenye kutekelezeka kwa manufaa ya wafanyakazi,” alisema Bachalla

Katibu wa TUICO mkoa wa Iringa na Njombe Ndg. Karim Bachalla akizungumza wakati wa kikao cha tathmini ya mpango mkakati wa chama, Januari 27, 2021, Morogoro | Venance Majula/TUICO

Sangeze amewapongeza makatibu na watendaji wote kwa kazi nzuri iliyopelekea mafanikio ya kuridhisha ambayo yamekifikisha chama hapa kilipo.

Related

Regional 8120799353580714515

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress