Mfanyakazi wa Karne ya 21

 

Wakati idadi ya watu wanaofanya kazi barani Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa watu milioni 450 ifikapo 2035 (Sasa ni milioni 440 - Benki ya Dunia), uchumi wa kidigitali pia unazidi kukua. Hapa tunamaanisha, uchumi ambao unategemea teknolojia ya kompyuta. Kwa maneno mengine – uchumi wa kimtandao.

Kwa hivyo, tunaweza kusema kuwa mfanyakazi wa karne ya 21, ni ‘binadamu mpya’ kwenye uchumi mpya. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya ulimwengu wa kazi, ambapo tuna ufikiaji mkubwa wa zana za kiteknolojia ambazo zinampa kila mmoja wetu sauti nje ya kuta za makampuni au taasisi za kazi. Lakini pia tunapata taarifa na kuna mwingiliano baina yetu kikazi.

Siku hizi kila mmoja anaweza kutumia mtandao kutafuta kazi, kusoma sheria na kanuni mbalimbali za kazi lakini pia tunasoma maoni ya watu wengine mtandaoni. Hii inamaanisha kwamba, nje ya mazingira ya kazi, tayari tuna sauti na tunaweza kushiriki hisia zetu wakati wowote. Mwajiriwa unaweza kujua haki na majukumu yako kisheria kwa kutumia mtandao wa intaneti hata kama kazini kwako hakuna hizo sheria.

Kwa mfano, janga la Covid-19 limetufundisha sisi sote kwamba licha ya kuwa na ulimwengu wa mwili, pia tuna ulimwengu mtandao na tunahitaji kuwa na uelewa wa matumizi ya zana za kidigitali. Ni wakati wa janga hili, karibu kila kampuni imetumia majukwaa ya mikutano ya video kama Zoom, Skype au Hangouts za Google kufanya mikutano. Vyama vya wafanyakazi pia vilitumia mtandao kufanya shughuli tofauti za uhamasishaji na elimu kwa wafanyakazi.

Hivyo, katika karne hii ya 21, tunahitaji kujitenga na mifumo tuliyoizoea ya kimenejimenti ili tuweze kukonga mioyo na akili za wafanyakazi ambao wanataka kufanya kazi zao za maisha. Kuhusu wale ambao bado hawajapata elimu ya kidigitali, sisi sote tunawajibika kuchambua mwenendo wa kazi duniani na kuwaimarisha wafanyakazi wote kwa kile kinachotokea katika ulimwengu wa kazi na maisha - mambo yanabadilika jamani.

Haya yote yatafanikiwa kwa uwekezaji wa mitaji iliyolengwa vizuri kwenye rasilimali watu na vitu. Lakini pia sera zinazokuza ushindani, elimu ya kiditali pamoja na uzalishaji wenye tija. Nguvu kazi kubwa ya Afrika ambayo ni vijana, ina uwezo wa kubadilisha bara hili kwa kiwango kikubwa na kusababisha ajira zenye staha kwa wote. Mshikamano Daima.


Related

Recent News 7827567542129959134

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress