Dondoo Muhimu za Uhamasishaji na Uelimishaji wa Wafanyakazi


Baadhi ya ‘nondo’ kutoka kwa mwezeshaji katika semina ya mafunzo kwa wakufunzi, Mwalimu Fredrick Mng’ong’o, Mkuu wa Idara ya Elimu na Uimarishaji TUICO Makao Makuu.

Mkuu wa Idara ya Elimu na Uimarishaji Fredrick Mng'ong'o akiwezesha katika semina ya mafunzo kwa wakufunzi inayoendeshwa na TUICO kwa ushirika na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Vyama vya Wafanyakazi (DTA), Dar es Salaam.


     
Mwalimu anasema, huwezi kuwaelimisha wafanyakazi kama huna mpango kazi wa mafunzo yako kwa wafanyakazi. Mwongozo ndio unaokupa kufikia malengo yako.

·      Na katika kutengeneza mwongozo huo wa mafunzo hakikisha unafahamu mahitaji ya wafanyakazi kwenye eneo la kazi. Je, kuna changamoto gani? Wanataka kufahamu nini kwa wakati huo?

·     Anasema utafahamu mahitaji ya wafanyakazi kwenye eneo lao la kazi kwa kufanya mahojiano na wafanyakazi hao au watu wanaoishi maeneo ya karibu.

Lakini, sio tu kuwahoji,  pia unaweza kufanya utafiti wako kwa kusoma nyaraka mbalimbali za eneo la kazi mfano mikataba na sera za kazi kwenye eneo hilo au kwa kushiriki chakula kwenye eneo la kazi


Mwalimu Mng’ong’o anaendelea kusema;-

Katika kutengeneza mbinu za kufundishia, inategemea na aina ya maudhui na malengo ambayo mkufunzi umejiwekea. Lazima uzingatie umri wa wafanyakazi, eneo la kufundishia, idadi yao, muda, mada na vifaa wezeshi.

 

 “Utakavyowahamasisha au kuwafundisha wafanyakazi wanaosimika nguzo za umeme kwa mfano, ni tofauti na utakavyowafundisha wahasibu kwenye taasisi fulani,” Mwalimu Mng’ong’o 

 Lakini pia, anasema, ni jambo la muhimu sana kwa mkufunzi kuzingatia muda anaopewa na mwajiri fulani kutoa elimu ya mfanyakazi. Kama umepewa saa moja la kufundisha wafanyakazi, hakikisha umepangilia mambo yako vizuri na uende moja kwa moja kwenye hoja kwa sababu tayari unafahamu mahitaji ya wafanyakazi. Na ni lazima kila kipengele utakachofundisha kipewe muda wake maalumu usije ukajikuta umetumia muda mrefu kwenye utangulizi peke yake.

Semina ya mafunzo kwa wakufunzi inaendelea jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya uhamasishaji na uelimishaji kwenye maeneo yao ya kazi ikiwa ni mkakati wa TUICO kupanua wigo wake katika kuwafikia wafanyakazi wengi nchini.

 

Related

Recent News 8581664963262424525

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress