TUICO Yaendesha Mafunzo kwa Wakufunzi

 

Dar es Salaam

Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Vyama cha Wafanyakazi la Denmark (DTA), wiki hii, kinafanya semina ya siku nne ya mafunzo kwa wakufunzi.Semina hiyo inayofanyika jijini Dar es Salaam, inatumia mbinu shirikishi za mafunzo, na inajumuisha mihadhara, majadiliano, kazi za vikundi, kutoa mawazo, mazoezi;  na inawawezesha wakufunzi kutoka TUICO Makao Makuu kuwafundisha washiriki (ambao wanakuwa wakufunzi kwenye maeneo yao ya kazi) kuhusu haki za wafanyakazi, elimu ya msingi ya vyama vya wafanyakazi, elimu ya masuala ya jinsia, Afya na Usalama Kazini, mikataba ya hali bora na kushughulikia malalamiko.

Mafunzo hayo yanajumuisha washiriki kutoka Serengeti Breweries Limited, Kampuni ya Coca-Cola, CRDB Bank Plc, MeTL Group, A-One Products and Bottlers Limited, Marie Stopes, Shirika la Masoko Kariakoo, NSSF, TGDC, TANESCO, TPB Bank Plc, TUICO (Kinondoni, Temeke na Ilala) Dar es Salaam.


Kupitia semina hiyo ya siku nne, TUICO inakusudia kupanua wigo wake katika kuhamasisha wafanyakazi kujiunga na chama na kuwafikia kwa wingi katika maeneo yao ya kazi na washiriki wanafundishwa kuhusu namna ya kukusanya habari juu ya mahitaji ya mafunzo, uundaji wa malengo ya mafunzo, kuelewa mahitaji ya wafanyakazi, chaguzi za mbinu za mafunzo na vifaa vya mafunzo. 

Related

Recent News 1694172362826909339

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress