TUICO YAPITIA UPYA SERA YA JINSIA

 

Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kimefanya marejeo ya sera yake ya jinsia ikiwa ni kuitikia mabadiliko yanayotokea katika mifumo ya maisha kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa, kijamii na kiutamaduni.

Jovita Mlay, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SASA Foundation akiwasilisha moja ya mada zake katika semina ya kutazama upya Sera ya Jinsia ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) iliyofanyika Aprili 08-09, 2021, Morogoro.

Katika semina ya siku mbili mkoani Morogoro, TUICO kwa kushirikina na Friedrich Ebert Stiftung (FES-Tanzania) na wadau mbalimbali wa masuala ya jinsia pamoja na Kamati ya Wanawake ya TUICO ilipitia upya sera ya jinsia na kubaini masuala mbalimbali:-

Mosi, ubaguzi wa kijinsia katika maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda, mashirika, biashara katika sekta rasmi na isiyo rasmi na vyama vya wafanyakazi bado unadhihirika huku wanawake wakifanya kazi zenye kada ya chini na zenye ujira na utaalamu mdogo ukilinganisha na wanaume.

Baadhi ya washiriki wa semina ya kutazama upya Sera ya Jinsia ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) iliyofanyika Aprili 08-09, 2021, Morogoro.

Pili, bado kuna uelewa mdogo wa masuala ya kijinsia na mitazamo tofauti kuhusu usawa wa kijinsia hali inayorudisha nyuma juhudi za harakati kuelekea usawa huo.

Washiriki wa semina ya kutazama upya Sera ya Jinsia ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) iliyofanyika Aprili 08-09, 2021, Morogoro.

Tatu, bado mawazo mgando yanatawala maeneo ya kazi kuhusu uwezo wa mwanamke kitaaluma na hivyo kudidimiza ukuaji wa mwanamke kitaaluma na kiuongozi ukilinganisha na mwanaume.

Nne, uwiano kiungozi kwenye ngazi za maamuzi katika vyama vya wafanyakazi na mashirika bado umemwacha mwanamke nyuma kutokana na mzigo wa malezi usiozingatia usawa wa kijinsia na haki.

Tano, bado kuna changamoto kubwa ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono hasa kwa wanawake.

Sita, utambuzi kuhusu upana wa eneo la kazi hasa katika sekta iliyo rasmi unahitaji kutazamwa upya.

Saba, ukosefu au upungufu wa takwimu na taarifa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia na  kingono, kiwango cha uelewa wa jinsia na mikakati au njia zitakazotumika kushughulikia masuala ya unyanyasaji huo.

Maria Bange Mkuu wa Idara ya Wanawake TUICO Makao Makuu, akiwasilisha moja ya mada zake katika semina ya kutazama upya Sera ya Jinsia ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) iliyofanyika Aprili 08-09, 2021, Morogoro.

Sasa, TUICO itakuja na sera ya jinsia iliyoboreshwa zaidi na inayotoa suluhu ya maeneo yaliyobainishwa ili kukidhi mahitaji yanayotokana na mabadiliko katika mifumo ya maisha na kukuza ushiriki wa mwanamke katika uongozi, maamuzi lakini pia kujenga jamii yenye usawa wa kijinsia na inayothamini jinsi zote.

 

Related

Women 9131763917815436119

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress