Tunasherehekea Miaka 57 Ya Muungano


Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliundwa tarehe 26 Aprili, 1964 na ulizinduliwa rasmi na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na Hayati Sheikh Abeid Aman Karume, Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Waasisi hao walibadilishana Hati za Muungano na kuchanganya udongo wa Tanganyika na ule wa kutoka Zanzibar kama ishara ya muungano wa nchi mbili. Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania huku Sheikh Karume akiwa Makamu wa kwanza wa Rais.

Kanuni za Msingi za Muungano wa mwaka 1964 zinaeleza kwamba chimbuko la Muungano huu, pamoja na mambo mengine, linajumuisha uhusiano wa karibu na wa muda mrefu kati ya watu wa Tanganyika na Zanzibar, uhusiano wa kisiasa uliotokana na harakati za kupigania uhuru  zinazofanana na imani ya pamoja ya Uhuru wa Afrika yote.

Kwa mara ya kwanza, kwenye Bara la Afrika, iliwezekana kuungana kwa mataifa mawili huru yalikuwa yanajitawala. Tukio hili linaonesha dhamira ya dhati, ari na moyo wa watu wa Afrika na viongozi wao, kwamba, inawezekana kuwa na umoja wa Afrika. 

Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo umoja pekee ambao bado unaendelea miongoni mwa miungano adimu sana duniani kote. Muungano Wetu. Nguvu Yetu. Mshikamano Daima.

 

 

Related

Recent News 2695936009114911967

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress