MWANZA: ZAWADI KWA WAFANYAKAZI NA WAAJIRI BORA

http://www.tuico-union.org/2021/05/mwanza-zawadi-kwa-wafanyakazi-na.html
Baada ya Maadhimisho ya Mei Mosi, TUICO Mkoa wa Mwanza waliandaa hafla ya kutoa zawadi kwa wafanyakazi na waajiri bora. Katika hafla hiyo Mwenyekiti wa TUICO Taifa Ndg. Paul Sangeze alikuwa Mgeni Rasmi. Sangeze aliambatana na Katibu Mkuu wa TUICO Ndg. Boniface Nkakatisi, Naibu Katibu Mkuu Ndg. Tamim Salehe, Mkuu wa Sekta y a Huduma na Ushauri Bi. Margaret Ndagile pamoja na viongozi mbalimbali kutoka TUICO Makao Makuu na Mkoa wa Mwanza.