TUICO INATAMBUA MCHANGO WA VYOMBO VYA HABARI ULIMWENGU WA KAZI

 

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini wakati wa maadhimisho ya siku ya afya na usalama mwaka 2021 yaliyofanyika uwanja wa Nyamagana, Mwanza | Picha na TUICO

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari, mwaka huu 2021, Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi zza Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), kinatambua mchango wa vyombo vya habari katika harakati za kutetea na kulinda haki, heshima na maslahi ya wafanyakazi nchini. 


Vyombo vya habari ni wadau wetu wakubwa katika harakati za kupigania haki, heshima na maslahi ya wafanyakazi nchini. 

Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu inayosisitiza kuhusu HABARI KWA MASLAHI YA UMMA — Hivyo, wakati umefika kwa wanahabari kutazama zaidi kwenye changamoto wanazokutana nazo wafanyakazi na kuwasadia kupaza sauti. 

Ni ukweli usiopingika kwamba, vyombo vya habari vinahitaji uhuru, ufanisi na nafasi ili vitekeleze majukumu yake kwa maslahi ya umma hasa tabaka la wafanyakazi. 

Aidha, vyombo vya habari ni muhimili muhimu katika kuleta maendeleo ya watu, demokrasia na haki za wafanyakazi ambazo ni haki za binadamu.

Vyombo hivi, vinachagiza uwajibikaji na uwezeshaji. Ni jukwaa la mijadala na elimu mbalimbali yenye maslahi kwa umma hasa wa wafanyakazi.

Tunawatakia maadhimisho mema ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari.

 HABARI KWA MASLAHI YA UMMA!

Related

Recent News 7060516343568081847

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress