Kamati ya Vijana TUICO-Taifa 'Yapigwa Msasa'

Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo Sangeze amewaasa vijana kuja na mipango mkakati ili wakisaidie Chama huku akiwasisitiza kusoma maandiko muhimu ya Chama ikiwa ni pamoja na Katiba ili wawe na taarifa sahihi za Chama.
“Tunawategemea mje na hoja na mipango madhubuti ya kukisaidia Chama. Vijana someni Katiba ya Chama. Chama kinawategema sana katika kazi kubwa ya kuwahamasisha vijana,” amesema Ndg. Sangeze
Awali akizungumza katika semina hiyo Katibu Mkuu wa TUICO Ndg. Boniface Nkakatisi ameelezea umuhimu wa Semina na vikao vya Kamati ya Vijana TUICO-Taifa.
“Katika semina na vikao kama hiki ndipo mnapojadili mambo ya vijana na nafasi yenu huko mliko na hata kitaifa. Mambo mnayozungumza hapa maana yake mnapeleka kwa Katibu Mkuu kwa ajili ya kutazama utelekezaji kwa yale yanayowezekana na sio ya kusadikika,”
“Tunapokutana kitaifa namna hii ndipo mahala mnachati halafu yanakwenda mpaka kwa wenzenu walioko mikoa mingine kwa sababu sio mikoa yote imeleta wajumbe hapa,” amesema Katibu Mkuu Nkakatisi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana TUICO-Taifa Ndg. Allen Lyimo amehakikisha ushiriki wa vijana katika ujenzi wa Chama ikiwa ni pamoja na kufumbata mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Amesema watatumia maendeleo ya Tehama kuhamasisha wafanyakazi hasa vijana ambao hawako kwenye Chama wajiunge kwani ni suala muhimu utuo kwa mfanyakazi yeyote kuwa ndani ya chama cha wafanyakazi.
Kesho Novemba 06, 2021, Wajumbe
wa Kamati ya Vijana TUICO-Taifa wataendelea na Kikao cha Kamati ya Vijana
ambacho ni kwa mujibu wa Katiba ya Chama.