TUICO yajengea uwezo viongozi wa matawi

Kwa kushirikiana na IndustriALL Global Union, TUICO tumewajengea uwezo viongozi wa matawi kutoka Mazava Fabrics and Production EA Limited, Wilmar Rice Tanzania Limited na 21st Century Textiles Limited mkoani Morogoro.

TUICO kina shauku ya kuwa na viongozi wa matawi wanaoweza kutatua migogoro ya kikazi inayojitokeza maoneo ya kazi, waingie kwenye kamati za majadiliano sambamba na kuhamasisha na kuingiza wanachama: kisha, kuona mikataba ya hali bora za kazi inasainiwa kati ya TUICO na makampuni mbalimbali.

Vile vile, ili kujenga ulimwengu wa kazi ambao ni salama na wenye haki, wafanyakazi lazima watambue kuwa unyanyasaji wa kingono ni uvunjifu wa haki za binadamu. Chama kimeendelea kuchagiza sera madhubuti dhidi ya unyanyasaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha mifumo rafiki ya kuripoti visa vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na kingono.

Semina hii imewaibua viongozi wa matawi katika simulizi na mifano tofauti kuhusu namna ya kushughulikia migogoro kwenye maeneo ya kazi, viwango vya ajira, afya na usalama kazini, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na kingono, uhamasishaji na elimu ya vyama vya wafanyakazi

Related

Seminars and Workshops 6290666513033430971

Post a Comment

emo-but-icon

TUICO CAMPAIGNS TO END GBV

ABOUT TUICO

TUICO on Twitter

TUICO ON FACEBOOK

Connect Us

item
Wordpress